• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS SAMIA atoa zaidi ya shilingi trilioni mbili kutekeleza miradi mbalimbali Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: April 7th, 2023

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili madarakani imetoa zaidi ya shilingi trilioni mbili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa  Ruvuma Kanali Laban Thomas  aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Wakili Julius Mtatiro wakati anatoa salamu za Mkoa wa Ruvuma kwenye Ibada ya Kitaifa ya Ijumaa Kuu  ambayo  imefanyika katika Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi  la KIUMA wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Kanali Thomas amesema kati ya fedha hizo katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2023 kwa wilaya ya Tunduru pekee,serikali ya Rais Samia imetoa zaidi ya shilingi bilioni 223 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

“Kati ya shilingi bilioni 223 zilizotolewa kwa Wilaya ya Tunduru pekee,shilingi bilioni 150 zinaendelea kujenga mradi msongo mkubwa wa umeme kutoka Songea hadi Tunduru,unaweza kuona Tunduru ni eneo la pembezoni hata hivyo serikali imetenga mabilioni kuhakikisha umeme wa uhakika unafika Tunduru’’;allisema RC Thomas.

Hata hivyo amesema miradi yote inatekelezwa na serikali kwa kuwa watanzania wanalipa kodi ambapo amesisitiza kulipa kodi ni wajibu wa kila mtanzania.

Kanali Thomas amewakumbusha wananchi kuweka akiba ya chakula katika kipindi hiki cha kuelekea mavuno ili familia zisipate upungufu wa chakula iwapo watauza chakula chote.

Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa wakati wakristo wanaadhimisha mateso na kifo cha Yesu Kristo  siku ya Ijumaa Kuu ametoa rai ,kuendelea kudumisha amani,umoja,mshikamano na utulivu  wa Taifa letu.

Amesema Taifa na kanisa la Mungu litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwa amani  na utulivu vilivyopo hapa nchini ni msingi wa kila jambo ambapo ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwa mamlaka zinazohusika pale wanapoona jambo lolote linalihatarisha amani ya nchi.

Amesema wakati wakristo wanaadhimisha mateso ya Yesu Kristo,ni muhimu watanzania kuwa na upendo kwa watu wote kama alivyofanya Yesu Kristo hivyo Kanisa la Mungu na watanzania kwa ujumla katika kipindi hiki litafakari kuhusu upendo wa kweli ambao unazaa kila kinachoonekana.

Akizungumzia kuhusu mmomonyoko wa maadili ambao unaendelea katika mataifa mbalimbali Duniani,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema mmomonyoko huo umetokana na wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kushindwa  kusimamia kikamilifu maadili ya vijana wao.

Ametahadharisha kuwa  mmomonyoko wa maadili unaendelea kutishia usalama wa taifa letu  ambapo amewataka wazazi na walezi kuwajibika katika malezi ya vijana wao huku akiwataka vijana kuacha kufuata utamaduni wa kishetani.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni  Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Mhashamu Raphael Haule akizungumza kwenye Ibada hiyo  ametoa rai kwa wazazi na walezi wa Tanzania kuwaleta Watoto wao katika misingi ya dini na maadili ya Tanzania.

Mhashamu Haule amesisitiza kuwa wazazi wakitekeleza wajibu wao vizuri Taifa la Mungu litakuwa salama ambapo ametoa rai kwa madhehebu yote kushirikiana kwa kuunganisha nguvu ili kuliokoa Taifa la Mungu na kuiponya jamii ya kitanzania hasa katika kipindi hiki cha mmomonyoko wa maadili.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Aprili 7,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.