Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ametangaza rasmi ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuwasili mkoani Ruvuma tarehe 30 Julai 2025 kwa ziara ya siku moja, yenye lengo la kuzindua mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya uranium katika Wilaya ya Namtumbo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Songea, Kanali Ahmed amesema mradi wa uchimbaji wa uranium wilayani Namtumbo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati nchini, unaotarajiwa kuchangia pato la taifa kupitia kodi, kutoa ajira kwa wananchi na kuleta maendeleo ya miundombinu, hivyo kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.
Amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu umuhimu na fursa zitakazopatikana kutokana na uwepo wa mradi huo.
Vile vile amewataka kuendelea kushirikiana na ofisi yake na ofisi za wakuu wa wilaya ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi huku wakihamasisha utulivu, mshikamano na uzalendo miongoni mwa wananchi ili siku hiyo iwe ya historia njema kwa mkoa wa Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.