KATIBU Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki akiwa na Menejimenti Mkoa amefanya ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili yaliyogharimu shilingi milioni 40 katika shule ya sekondari Makita iliyopo Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Hata hivyo taarifa ya taaluma ya sekondari hiyo katika matokeo ya kidato cha nne imemsikitisha Katibu Tawala huyo baada ya kuelezwa kuwa wanafunzi 85 kati ya wanafunzi 174 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2022 wamepata daraja la nne na sifuri ni zaidi ya nusu ya darasa
kulingana na Baraza la Mitihani matokeo ya kidato cha nne mwaka 2022 katika sekondari hiyo yanaonesha kuwa daraja la kwanza wapo 11,daraja la pili 33 daraja la nne 80 na sifuli watano
Ndaki amewataka walimu wa shule hiyo ambao ni zaidi ya 47 kufundisha kwa bidii ili wanafunzi wengi waweze kufaulu mtihani wa kidato cha nne ambapo ametahadharisha kuwa katika mtihani wa mwaka huu hataki kusikia hali hiyo inajirudia tena vinginevyo atachukua hatua kali.
Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma akiwa na Timu ya Menejimenti Mkoa wa Ruvuma wapo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.