Na Gustaph Swai- Rs Ruvuma
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo ametahadharisha kuwa takwimu zisizo sahihi zinaweza kusababisha upotevu wa rasilimali na kuchelewesha maendeleo yanayotakiwa kuonekana katika jamii
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) Ulioboreshwa kwa Waratibu wa Mfumo huo kwa Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
"Takwimu zisizo sahihi zinaweza kusababisha upotevu wa rasilimali na kuchelewesha maendeleo tunayotamani kuyaona katika jamii", Alisema.
Amewataka Waratibu hao kutoa takwimu sahihi na kufanya kazi ili kuwa na taarifa zilizo sahihi kwani matarajio kuanzia ngazi ya Taifa hadi Msingi ni makubwa na wananchi wanahitaji maendeleo.
Amewaagiza wataratibu kuandaa taarifa mapema, kuzikamilisha na kuziwasilisha kwa wakati na kufanya kazi kwa weledi kwani bila ya kuwa na taarifa ni sawa na kutokufanya kazi na kushindwa kuwajibika jambo ambalo ni kosa.
Ametoa rai kwa Waratibu hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani hali hiyo inachelewesha kufikiwa kwa malengo ya Serikali na kuwakosesha Wananchi maendeleo na kuwataka kubadilika na kujipanga vyema kufanya kazi kwa ufanisi.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa Mfumo wa fursa na vikwazo ulioboreshwa ni moja ya juhudi zinazofanywa na Serikali kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wananchi ili Kuwaongezea ari ya ushiriki kwa kupanga na kusimamia shughuli za maendeleo.
Amelitaja lengo la maboresho ya Mfumo huo kuwa ni kuhakikisha wanaweza kutatua changamoto zilizokuwa katika mfumo wa awali kama vile ushiriki hafifu, jamii kukosa Moyo wa umiliki wa miradi na kuongezeka kwa utegemezi wa jamii kwa Serikali.
Amesema mfumo huo ni nyenzo muhimu katika mchakato wa maendeleo ya jamii zetu hivyo unatarajiwa kuleta faida za Moja kwa Moja katika kuleta utoaji wa huduma na maendeleo endelevu.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Ndg.Jumanne Mwankhoo amewasisitiza Waratibu kubadilika na kujenga Utamaduni wa kufanya kazi bila kuhimizwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.