Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo ameziagiza Halmashauri zote nane kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi kwa ufanisi zaidi.
Agizo hilo limetolewa katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea, lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Lindusi. Katika kikao hicho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma aliwakilishwa na Amina Tindwa.
Katika hotuba yake, Tindwa alisisitiza kuwa taasisi zote za umma zinapaswa kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa mujibu wa maelekezo kutoka TAMISEMI na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Alisema kuwa hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuimarisha uwajibikaji wa watumishi wa umma.
Aidha, Tindwa ameagiza kuanzishwa kwa ofisi maalum za malalamiko katika halmashauri zote, ili kusaidia Serikali kusikiliza na kutatua kero za wananchi waliowachagua viongozi wa umma.
Amelitaja lengo la kushughulikia kero za wananchi ni kupunguza manung’uniko na kuhakikisha kuwa serikali inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na uwajibikaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.