MGOMBEA MWENZA nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhemishiwa Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Ruvuma kuanzia Septemba 14 mwaka huu ambapo ameanza ziara yake katika wilaya ya Tunduru na Namtumbo.Kulingana na ratiba ya ziara yake mkoani Ruvuma,Septemba 15 mwaka huu atakuwa wilaya ya Songea asubuhi atakuwa Madaba katika uwanja wa Lembuka A na jioni atakuwa Matarawe Manispaa ya Songea katika uwanja wa michezo shule ya msingi Matarawe.
Kulingana na ratiba hiyo Septemba 16 mwaka huu,asubuhi atakuwa Peramiho kwenye uwanja wa tamasha,mchana atakuwa Mbinga uwanja wa michezo wa nyoni na jioni atakuwa Mbinga mjini kwenye uwanja wa michezo wa CCM.Ratiba hiyo itamalizika wilayani Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma siku ya Septemba 17 asubuhi atakuwa Liuli kwenye uwanja wa michezo wa mji wa Liluli na mchana atakuwa uwanja wa mazoezi wa jeshi la polisi mjini Mbambabay.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.