MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amekutana na wadau wa Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kujadili changamoto mbalimbali za moto zinazojitokeza.
Mkuu wa Wialaya ya Songea Wilman Ndile amemwakilisha Mkuu wa Mkoa katika Kikao hicho cha wadau wa Misitu kilichofanyika Katika Ukumbi wa Amani na kuhudhuria wadau mbalimbali.
Ndile akizungumza katika kikao hicho amesema Misitu ni maisha ya watu ikiwa baadhi ya Halmashauri wanaishi kwa kutengemea Misitu ikiwemo Halmashauri ya Mufindi na Mafinga Mkoa wa Iringa.
“Halmashauri hizo wanakipato cha kujitocheleza kutokana na Misitu ikiwa madaba tunalima mazaoya chakula na misitu”.
Amesema miaka 20 iliyopita Madaba hapakuwa na ajenda ya Misitu wala TFS haikuwepo wala miti iliyokuwepo haikuwa ajenda ya kibiashara.
“TFS katika Halmashauri ya Madaba wataanza kuvuna Mazao ya Misitu siyo mda mrefu na mapato yataongezeka sana ikiwa Halmashauri inakusanya Bilioni 1ya mapato ya ndani “.
Hata hivyo Ndile amesema swala la uchumi wa Misitu ni maisha ya watu,na Nchi ikiwa sawa na uchumi mwingine kama dhahabu Geita.
Hivyo Mkuu wa Wilaya ameagiza kutunza Misitu kikamilifu bila kuchoma moto holela hata misitu ya asili watakaobainika wanachoma moto wachukuliwe hatua kali ya kishelia.
“Wiki mbili zilizopita tumepata wawekezaji kutoka Ulaya wamesaini Mkataba katika Mkoa wa Ruvuma akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru na Namtumbo mkataba unasema vijiji vitakavyotunza msitu vizuri watapewa fedha za asante kwa kutunza misitu “.
“Kama moto unasababisha madhara makubwa lazima tushughulike nao ndiomana sisi ni viongozi tumeona tuanze na hilo kila mmoja awe na ajenda ya miaka ijayo ili janga la moto lisitokee”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.