Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyasa kuhakikisha wote waliohusika na wizi wa vifaa vya miradi ya maji Kata ya Lituhi na Liuli wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kanali Thomas ametoa agizo kufuatia kusomewa taarifa ya wizi wa vifaa vya miradi ya maji Lituhi na Liuli katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi hiyo aliyoifanya juzi.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 11 kutekeleza miradi hiyo miwili katika Wilaya hiyo.Miradi yote mwili inatarajia kukamilika Aprili 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.