• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC ABBAS tunakwenda kuwa na uhakika wa uzalishaji Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: September 12th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Mkoa huo unakwenda kuwa na uhakika wa uzalishaji kupitia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia zoezi la kupima na kujua afya ya udongo linalofanyika mkoani humo kwa kuwawasaidia wakulima kujua ardhi yao inapungukiwa na virutisho gani, aongeze nini ili aweze kupata mazao kulingana na afya ya udongo inavyoelekeza.


Kanali Ahmed Abbas amesema hayo mapema wiki hii wakati wa zoezi la upimaji wa afya udongo linaloendelea mkoani humo ambalo litadumu kwa taribani wiki nne na kueleza kuwa Mkoa huo unajivunia sana jitihada kubwa zinazofanywa na Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia  wataalam wa kilimo vifaa vya kupimia afya ya udongo na pikipiki kutekeleza majukumu yao.


“Zoezi hili la kupima afya ya udongo na vifaa  vingine vingi ambavyo vipo vinakwenda kuwa mkombozi  kwa wakulima wetu kwa maana hiyo sasa kilimo kinaweza kuwa uti wa mgongo kama ilivyokuwa ikizungumzwa zamani kwasababu tutakuwa na uhakika wa kile tunachokizalisha." ameongeza RC Ahmed Abbas Ahmed.


Sambamba na hilo, Kanali Ahmed Abbas amesema Mkoa huo unajivunia bei nzuri za mazao ya mahindi ambapo kwa kilo moja imefikia kununuliwa kupitia NFRA shilingi 700 pamoja na kusogeza karibu huduma za kimalipo kwa wakulima.


Nae Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Eng. Juma Omary Mdeke amesema Wizara ya Kilimo inaendesha zoezi la kupima afya ya Udongo nchi nzima na zoezi hilo limeanzia katika mkoa wa Ruvuma ambapo wataalamu hao watapima udongo katika Wilaya na Kata zote za Mkoa huo ili kuweza kutengeneza ramani ya afya udongo kuonesha hali ya udongo katika maeneo husika ambayo yatasaidia sana katika kutambua ni mazao gani yalimwe na matumizi sahihi ya mbolea.


"Lengo kuu ni kutaka kuhakikisha tija ya wakulima inaongezeka katika maeneo mbalimbali ambayo yanafanyiwa kazi hiyo na tukumbuke Wizara ya Kilimo ina ajenda muhimu kabisa ajenda ya 10/30 ambayo tunaitekeleza kwa vitendo ili kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030." amesema Eng. Mdeke.


Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya ardhi ya kilimo kwa kuendelea na zoezi la kutambua na kupima afya ya udongo kwa nchi nzima ili kuandaa ramani ya udongo ya nchi nzima inayoonesha hali ya udongo, katika zoezi hilo mikoa mitatu (Ruvuma, Lindi na Mtwara) itakuwa ya mwanzo kwa ajili ya kufanyiwa zoezi hilo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.