Pichani mwenye kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa na Kamati ya Usimamizi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Chief Zulu Academy inayojengwa katika kata ya Mshangano mjini Songea kwa gharama ya shilingi milioni 500.
Mkuu wa Mkoa amempongeza Msimamizi Mkuu wa mradi huo ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Luhira Mwl Oreda Ng’oro pichani wa pili kutoka kulia ambaye amewezesha hadi sasa kutumika shilingi milioni 290 kutekeleza mradi huo .
Mkuu wa Mkoa amepongeza Usimamizi wa kizalendo uliofanywa na Mwalimu huyo huku akiwashauri wanaosimamia miradi ya serikali kufika kujifunza kwenye mradi huo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.