MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amefanya ziara ya ukaguzi wa maghala ya kuhifadhia mbolea yaliyopo Manispaa ya Songea.
Akizungumza katika ziara hiyo ameagiza kuanzia sasa wafanyabiashara wafuate bei elekezi ya mbolea ambayo ni shilingi laki moja na elfu tano na kwamba kuuza mbolea hizo kwa bei ya juu ni kinyume cha sheria.
RC Ibuge ameagiza wananchi wote waliolipishwa mbolea kwa bei ya 138,000 kwa mfuko wa kilo 50 warejeshewe fedha zao kwenye maduka ambayo walinunua mbolea hizo ‘’,alisisitiza.
Amesisitiza kuwa kupanda kwa bei ya mbolea kunatokana na kuagiza toka nje ya nchi na kwamba dunia nzima inahitaji mbolea hizo hivyo bidhaa inapotakiwa na wengi bei inapanda na kwamba sio kweli kwamba serikali imepandisha bei.
Hata hivyo amesema serikali imeweka mpango mzuri wa wa kitoa kibali kwa waagizaji ambao wanaleta mbolea nchini na kwamba katika Mkoa wa Ruvuma kuna maghala ya kutosha ya kuhifadhia mbolea za aina mbalimbali.
Hata hivyo amesema kuanzia msimu ujao wa kilimo bei ya mbolea nchini inatarajiwa kushusha kutokana na serikali kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea za aina mbalimbali jijini Dodoma.
Pia, RC Ibuge amesikiliza kero za wananchi wa Mtyangimbole na amewataka waache ubaguzi na matabaka baina yao juu ya umiliki wa ardhi kwani wote ni Watanzania hivyo wawe na umoja.
‘’Kila mamlaka iwe ya Kijiji au Halmashauri ina jukumu la kupanga mipango bora ya ardhi ya kijiji iko ili kuondoa matabaka na migogoro isiyo ya lazima ‘’, amesema RC Ibuge.
Aidha, amesema ni jukumu na ni wajibu wa serikali Tanzania pamoja na Vijiji vyake vyote viwe vimefikiwa umeme ifikapo Desemba 2022 hivyo wananchi wa Mtyangimbole wasiwe na wasiwasi katika swala la umeme.
Nae Mzee Komba mkazi wa Mtyangimbole amemuomba Mkuu wa Mkoa wakati wanapokuja kununua mahindi wakulima washirikishwe kwenye upangaji wa bei kwasababu wao ndio wanajua mahindi yamezalishwaje pamoja na gharama.
Mkoa wa Ruvuma kwa miaka mitatu mfululizo umekuwa kinara wa kuzalisha chakula nchini.
Imeandikwa na Bahati Nyoni
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma
Machi 18,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.