Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwa ameongozana na Waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko wamekagua mgodi wa madini ya Dhahabu wa Mwekezaji Mzawa Johnson Nchimbi uliopo katika kijiji cha Lukarasi Wilaya ya Mbinga.
Licha ya kumpngeza Mwekezaji Nchimbi kwa kuzalisha dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu na kuwezesha serikali kupata mapato ya zaidi ya shilingi milioni 200,Hata hivyo RC Ibuge amesema takwimu rasmi za uzalishaji wa dhahabu katika Mkoa wa Ruvuma zinaonesha uzalishaji unaendelea kushuka ambapo takwimu za Julai mwaka huu zinaonesha kuwa Mkoa mzima imezalishwa dhahabu kilo mbili tu suala ambalo amesema sio sahihi kwa kuwa Mkoa una uwezo za kuzalisha dhahabu nyingi hivyo kuongeza ajira na mapato kwa mtu binafsi na serikali.
TAZAMA HABARI KWA KINA HAPA https://www.youtube.com/watch?v=N-CV16LjM0Y
Kushoto pichani ni Waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Balozi Wilbert Ibuge wakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msalanja wakikagua mgodi wa dhahabu wa Nalasi wilayani Mbinga ambao unamiliwa na Mwekezaji binafsi Mtanzania Johson Nchimbi ambapo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi sasa umeweza kuzalisha dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu na kuwezesha serikal.i kupata mapato ya zaidi ya shilingi milioni 200
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.