MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kutoa mikopo kwa asilimia 100 yenye thamani ya tsh 66,600,000/- kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Amezitoa pongezi hivi karibuni katika mkutano maalum wa baraza la madiwani wa kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019/2020,wilaya ya Nyasa uliofanyika katika Ukumbi wa Kepteni John Komba Mbamba bay Wilayani Nyasa.
RC Ibuge amefafanua kuwa Kwa mara ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetoa mikopo kwa asilimia 100 kwa mchanganuo ufuatao, Wanawake milioni 37,600,000, vijana, 19,000,000 kundi la watu wenye ulemavu 10,000,000.
Pia ameipongeza Halmashauri kwa kufikia asilimia 82.95 ya lengo la kukusanya mapato ya ndani ya Tsh 1,475,667,800,hata hivyo imefanikiwa kukusanya Tsh 1,219,874,204,53, na ameitaka Halmashauri ya Nyasa kukusanya mapato kufikia asilimia 100 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2021.
“ninachukua fursa hii kuipongeza sana hii Halmashauri kwa dhati kabisa kwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh 66,600,000/= kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwa makundi hayo ni muhimu sana katika Uzalishaji mali”,alisema .
Aidha amewaagiza Madiwani na watendaji wa Halmashauri kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kuinua makusanyo na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mhe.Stewart Nombo ameahidi kutekeleza maagizo yote kwa maslahi ya wananchi.
Imeandaliwa na Netho Credo
Afisa habari Halmashauri ya Nyasa
Mei 21,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.