Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali “Balozi” Wilbert Ibuge amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Songea kwa kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 99.01%.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha baraza Maalum la Madiwani kilichofanyika leo 18 Juni 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kupitia taarifa za Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/2020, kikao kilichohudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 21 zilizopo katika Manispaa ya Songea, wakuu wa Idara na viongozi mbalimbali.
Akitoa pongezi hizo Ibuge amesema, Halimashauri ya Manispaa ya Songea katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 imekusanya kiasi cha Tshs. 3,374,756,150.90/= kati ya kiasi kilichotarajiwa kukusanywa ambacho ni Tshs. 3,408,416,455/= nakufikia lengo kwa asilimia 99.01%.
Alibainisha kuwa, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imechangia Tshs. 286,304,029/= ambayo ni sawa na asilimia 98.17% kwa ajili ya kuwezesha mfuko wa wanawake 4%, vijana 4% na watu wenye ulemavu 2%, fedha ambayo imesaidia kutoa fursa kwa vijana kujiajiri wenyewe pamoja na kuleta maendeleo kwa jamii.
Alisema “ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi Mkuu Mkazi wa hesabu za Serikali umetekelezwa vizuri na kufanikisha kujibu hoja zilizotolewa kwa zaidi ya asilimia 95% kati ya hoja zilizotolewa na kupelekea Halmashauri ya Manispaa Songea kupata hati safi. Pia Amewataka viongozi hao kuhakikisha wanamaliza kujibu hoja zote ambazo bado hazijakamilika kufungwa hadi kufikia tarehe 30 Septemba ziwe zimejibiwa. “ Aliwapongeza.”
Ametoa Rai kwa Waheshimiwa Madiwani na wataalamu kushiriki ipasavyo kujibu hoja zote pamoja na kutekeleza maelekezo wanayopewa kutoka kwa Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali wa ndani na kutoruhusu marudio ya hoja zilezile ambazo hujitokeza kila mwaka. “Ibuge Alieleza”
Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi katika kipindi cha kampeni na kusimamia vizuri miradi mikubwa iliyokamilika ikiwemo na stendi ya Tanga na machinjio ya kisasa ambayo imeanza kutumika ambapo inasaidia kuongeza mapato na kuleta maendeleo katika Halmashauri na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Ibuge ameziagiza Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanalipa madeni yote ya wazabuni kwa wakati, kuendesha vikao vya ukaguzi vya mapato ya ndani mara kwa mara kwa mujibu wa sheria. Wakurugenzi wote kila Halmashauri husika watahakikisha wanashiriki vikao vya ukaguzi pamoja na Waheshimiwa Madiwani ili kuleta ushirikiano wa pamoja na kutatua changamoto za Halmashauri husika.’Alisisitiza’
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema kuwa Baraza la Madiwani limejipanga kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Serikali katika kuhakikisha wanaleta maendeleo katika Manispaa ya Songea.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.