• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE awatahadharisha madiwani Namtumbo kuepuka migogoro

Imewekwa kuanzia tarehe: June 16th, 2021

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenarali Wilbert Ibuge, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuepuka migongano na mivutano isiyokuwa na tija  ambayo imekuwa chanzo kwa Halmashauri  kushindwa kutekeleza mipango yake,  na kusababisha wananchi  kukosa  baadhi ya huduma za kijamii.

Badala yake,  amewataka wajikite zaidi  kuijenga Halmashauri yao kwa kubuni vyanzo vipya na kuelekeza nguvu kubwa katika kukusanya na kusimamia mapato yanayopatikana ili kuharakisha maendeleo na uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

RC  Ibuge, amesema hayo jana wakati akizungumza na madiwani,watumishi na viongozi wa wilaya hiyo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi  mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Amesema, katika maisha ya kawaida hakuna binadamu wanaoweza kuishi bila kutofautiana kwa sababu mbalimbali,lakini kwa viongozi waliochaguliwa na walioteuliwa ni muhimu kumaliza tofauti  zao kwa maslahi ya wananchi na uhai wa Halmashauri yao.

“nilipoteuliwa na mwenye dhamana Mheshimiwa Rais Samiha Suluhu Hassan alinipa imani nije kumwakilisha  mkoa wa Ruvuma na sijiwakilishi mimi, nataka nisimamie maendeleo kwa kushirikiana na nyinyi”amesema.

Amesema, kutokana na ulezi wake kwenye Halmashauri za wilaya hataki kuona wala kusikia migogoro isiyokuwa na tija  kwa madiwani na  kuhakikisha wanamaliza tofauti zao,kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja.

Akizungumzia juu ya matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioshia tarehe tarehe 30 Juni 2020 amesema, Halmashauri ya Namtumbo haijafanya vizuri ikilinganishwa na rekodi  zinazoonesha kwa miaka minne iliyopita imefanya vizuri tofauti na hesabu za mwaka  wa fedha 2019/2020 baada ya kupata hati yenye mashaka.

Amesema, kwa mujibu wa taarifa za mkaguzi na mdhibiti  wa hesabu za Serikali(CAG)msingi wa kupata hati yenye mashaka ni kutokana na hati za madai zilizoidhinishwa kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato(LGRCIS)bila ya kuwa nyaraka toshelezi ambapo kiasi cha shilingi 191,935,660.00 hazijulikani zilipo.

Amesema, Halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka siyo jambo jema kwakuwa ina eneo kubwa kijiografia,wananchi wanaojituma katika shughuli za uzalishaji na hali ya hewa nzuri.Amesema, pamoja na kupata hati yenye mashaka, lakini hata  mwenendo wa kufanyia kazi taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali bado ni wa kusuasua.

Brigedia Jenerali Ibuge amesema, hali hiyo imejionesha kutokana na utekelezaji wa hoja na mapendekezo yaliyotolewa na CAG ambapo Halmashauri imeweza kufunga hoja 38 kati ya 100 za miaka ya nyuma,hivyo kusalia na hoja 62 kwa taarifa ya hesabu jumuishi.

Amesema, kuwepo kwa hoja nyingi  za CAG ambazo bado hazijafungwa na maagizo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambayo hayajafanyiwa kazi hadi sasa haitoi picha nzuri  na ishara kuwa menejimenti ya Halmashauri haizipi uzito unaostahili katika kujibu na hivyo kukosa majibu yanayotosheleza.

RC Ibuge ameagiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha inakamilisha utekelezaji wa kujibu maagizo ya kamati ya kudumu ya Bunge nah ja za ukaguzi ambazo bado hazijafungwa kabla ya tarehe 30 Septemba 2021.

Kwa upande wake mweka  hazina wa Halmashauri hiyo Pendo Nyomeye amesema, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kulikuwa na hoja 29,zilizofungwa 14 na 15 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sofia Kizigo amesema,katika wilaya hiyo kuna  vyanzo vingi,hata hivyo mapato yanayokusanywa hayalingani na vyanzo vilivyopo kutokana na baadhi yake kutoroshwa kwenda nje ya mfumo na mengine yanaishia kwa wajanja wachache.

Amesema, kupata hati yenye mashaka imeongeza ari ya kujituma na kufanya vizuri zaidi katika suala zima la kukusanya mapato na kuhaidi kufanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Imendikwa na Muhidin Amri,Mwandishi wa gazeti la serikali 

Juni 16,2021


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.