MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezitaka Halmashauri zihakikishe zinatoa elimu kuhusu mifumo ya masoko kwa wakulima na wadau wengine
Ameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa mfumo wa Stakabadhi Ghalani uliofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Songea
RC Ibuge amesema Halmashauri zihakikishe zinaweka usimamizi madhubuti wa vyama vya ushirika vya msingi na shughuli zote zinazohusu mifumo ya masoko hasa Stakabadhi Ghala.
“Wafanya biashara na wanunuzi wa mazao na vyama vikuu vya ushirika TAMCU na SONAMCU hakikisheni mnafanya malipo ya wakulima kwa wakati ili kufanya waupende mfumo huu vilevile muda wa kutekelezwa malipo uwe sehemu ya masharti ya ununuzi ”, amesema RC Ibuge.
Hata hivyo amesema uwekwe ukomo wa kiasi cha mazao yanayoweza kuuzwa nje ya mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuangalia nini kifanyike kuhusu wakulima wauze mazao machache wanayotaka kuuza na mengine kujikimu au kuhifadhi nyumbani.
Pia Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma zihakikishe zinaandaa mapema mipango na mikakati endelevu ya usimamizi wa zoezi la uzalishaji, ukusanyaji wa mazao na mfumo mzima wa masoko ya mazao hayo ili kumsaidia mkulima kupata kipato chake
Aidha, ametoa angalizo kwa wamiliki na wafanyabiashara wanaojishughulisha na kuhifadhi mazao kwenye maghala kuzingatia taratibu zilizowekwa katika uhifadhi wa mazao hayo watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa maghala yao.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni na Jackson Mbano
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
13 Mei 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.