• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE azindua chanjo ya UVIKO 19,asitisha mikusanyiko mikubwa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 4th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua chanjo ya UVIKO 19 kwa kuwa Raia wa kwanza  mkoani Ruvuma kuchanja chanjo hiyo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki alikuwa ni Raia wa pili kuchanjwa akifuatiwa na Kamati yote ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma.Wazee na viongozi mbalimbali wa dini pia walijitokeza kwa hiari kuchanjwa chanjo hiyo.

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Khanga amesema Mkoa wa Ruvuma wenye watu zaidi ya milioni 1.6  katika awamu ya kwanza umeletewa chanjo dozi 30,000.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa  Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  akizungumza kabla ya kuzindua chanjo hiyo ametoa rai kwa wananchi kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka na sabuni,kuvaa barakoa wakati wote wanapokuwa kwenye mikusanyiko na kutumia vipukusa mikono.

Hata hivyo amewashauri wananchi mkoani Ruvuma kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa hiari kwa kuzingatia sifa zilizoelekezwa na wataalam wa afya,kupata lishe bora na kufanya mazoezi.

“Kutokana na wimbi la tatu la UVIKO 19 katika Mkoa wa Ruvuma naelekeza viongozi wa ngazi zote waoneshe mfano kwa wananchi kwa kuchukua hatua za tahadhari za kujikinga dhidi ya  UVIKO 19’’,alisisitiza RC Ibuge.

Mkuu  wa Mkoa amewaagiza viongozi wa Taasisi zote wahakikishe wanasimamia upatikanaji wa vifaa kinga kama barakoa,maji tiririka na sabuni,pia ametoa rai kwa vyombo vya mawasiliano mkoani Ruvuma kutoa elimu kwa jamii kuhusu njia sahihi za kujikinga na UVIKO 19.

RC Ibuge ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha kuwa maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu kama stendi,bustani za kupumzikia,misikitini na makanisani kunakuwa na vifaa vya kunawia mikono.

Amewaagiza viongozi wa dini wahakikishe kuwa waumini wote wanavaa barakoa wakati wote wa Ibada na kukaa umbali usiozidi mita moja mtu mmoja hadi mwingine na kwamba Ibada ziwe  za muda mfupi usiozidi saa mbili na kwamba huduma zinazohusiana kugusana ziepukwe.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa kuanzia Agosti 4 mwaka huu amesitisha mikusanyiko yote mikubwa ya kijamii,kidini na kisiasa hadi ugonjwa utakapodhitibiwa na kutolewa taarifa rasmi na Wizara ya Afya.

Hata hivyo amesema mikusanyiko ya lazima,wananchi watalazimika kuomba kibali kutoka kwenye Mamlaka husika.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 4,2021

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.