MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua Operesheni ya uwekaji wa anwani za makazi na postikodi .
Uzinduzi huo umefanyika katika Manispaa ya Songea mara baada ya kikao na watendaji wote wa Mkoa huo, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa zoezi hilo muhimu.
Ibuge amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono yake na uamuzi wa kuanzisha operesheni muhimu kwa maendeleo ya Nchi kwa gharama nafuu.
“Kama mnavyokumbuka mwaka 2020 nchi yetu iliingia rasmi kwenye uchumi wa kati Kidunia turejee pongezi za dhati kwa Serikari ya awamu ya tano iliyoongozwa na Hayati Dr.John Magufuri”.
Hata hivyo Ibuge amesema kuna umuhimu wa kuondoka kwenye Ujima wa enzi za zama za mawe za kupigwa ngoma na kujulishwa ujumbe au taarifa na badala yake Taifa liingie kwenye Zama za Dunia ya kidijitali na Biashara Mtandao zinazojumuisha matumizi Makubwa ya Teknolojia ya Habari.
Amesema ili uchumi ukue kwa haraka na kuendelea kuwa Jumuishi kama ambavyo sasa Tafiti za Kimataifa zinaonesha kuwa Tanzania ni baina ya Nchi za Afrika zilivyokuwa kinara kwa Uchumi jumuishi ni lazima makazi na biashara ziweze kufikika kirahisi.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Ruvuma Ildefonce Ndemela amesema katika sekta ya Ardhi ni muhimu katika utekelezaji wa zoezi la mfumo wa Anwani za makazi na postikodi nchini.
Ndemela amesema mfumo huo ili uweze kuleta tija na ufanisi katika utoaji wa huduma lazima kuwepo na ramani zitakazotumika kuonesha maeneo mbalimbali ya miji na vijiji zizingatiwekwenye mfumo huo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Feburuari 15,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.