• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE azungumza na wazee wa Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 24th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameanza kukutana na makundi mbalimbali,kundi la kwanza kupata fursa hiyo ni wazee wa Mji wa Songea ambao wamewawakilisha wazee wa Mkoa wa Ruvuma.

RC Ibuge amezungumza na kusikiliza kero mbalimbali za wazee katika kikao kilichofanyika Ikulu Ndogo mjini Songea kikihusisha wazee wa makundi yote wakiwemo wazee wa Baraza la Makumbusho ya Majimaji,viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma.

Kabla ya kufanya majumuisho,Mkuu wa Mkoa alitoa fursa kwa wazee kutoa maoni yao na kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa jumla.

Mzee Ismail Nyingo  ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Makumbusho ya Majimaji,Mchungaji Adimu Mwezegule wa makanisa ya Pentekoste na Tito Mbilinyi, Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma walizungumzia changamoto ya Kituo Kikuu cha mabasi cha Songea kilichopo Kata ya Tanga.

Walisema licha ya kwamba Kituo hicho ni cha kisasa,changamoto kubwa ni abiria wanapofika kutoka nje ya Songea wanapata kero ya mawasiliano ya simu na daladala majira ya usiku hivyo kuingia gharama kubwa ya kukodi taksi hadi mjini Songea.“Tunaomba kwa usiku mabasi yanapofika stendi ya Tanga kuruhusu kubeba abiria hadi mjini  kwa sababu wananchi wanaangaika sana’’,alisema Mchungaji Mwezegule.

Mzee John Nyoni Mwenyekiti wa Baraza Huru la Wazee Manispaa ya Songea alimwomba Mkuu wa Mkoa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wazee zikiwemo Bima ya afya kwa wazee,pensheni na kuomba Sera ya wazee itungiwe Sheria kwa sababu ipo muda mrefu.Mayasa Mfaume ni Katibu wa Waganga wa Jadi aliomba kutatuliwa changamoto zinazowakabili waganga wa jadi alidai kwamba hivi sasa hakuna mfumo kamili wa kuwatambua waganga wa jadi na kuwapatia vibali.

Sponsioza Katambala amemuomba Mkuu wa Mkoa kukutana na mabaraza ya wazee mara kwa mara ili wazee hao waweze kuibua mambo mengi yanayohusu wazee  na wananchi kwa ujumla.Mzee Gerold Haule amemuomba Mkuu wa Mkoa kushughulikia pembejeo kwa wakulima ambapo amesema Mkoa umekuwa unazalisha kwa wingi mazao ya chakula kwa kutumia mbolea hivyo upatikanaji ukiwa rahisi uzalishaji unaweza kuongezeka zaidi.

Mzee Adolf Kumbukuru amezungumzia changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Mto Ruvuma ambao upo kwenye tishio kubwa kukauka kutokana na shughuli za kibinadamu.Ameomba  Mto huo kuhifadhiwa ili kuulinda.

Akizungumza baada ya kusikiliza changamoto za wazee,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema wazee ni hazina kubwa ndiyo maana ameamua kuwa kundi la kwanza kuzungumza nao baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa mkoa.RC Ibuge ameahidi atazifanyia kazi changamoto hizo,ikiwemo stendi ya mabasi ya Tanga ambayo amesema atafuatilia kwa sababu serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni sita kuwekeza na kwamba ataangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto za stendi hiyo bila kuathiri stendi.

Amesema changamoto zote atazifuatilia na kuzitolea majibu katika kikao kingine ambacho atapanga tena kukutana na wazee ambapo ametoa rai kwa wazee kuendelea kushirikiana na serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani katika mazao ya ufuta na soya,Mkuu wa Mkoa amesema mahitaji ya soko kupitia mfumo huo ni makubwa  hasa nje ya nchi na kwamba changamoto za mfumo huo ni ndogo kwa kuwa mkulima anapata faida kubwa zaidi.

“Kinachofanya maendeleo yasitokee popote ni wachache wenye maslahi binafsi ambao wanapotosha,mfumo wa stakabadhi ghalani tangu umeanza kutumika mkoani Ruvuma mwaka 2018,umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima’’,alisisitiza RC Ibuge.

Mkuu wa Mkoa pia amesisitiza suala la amani kuwa ni moja ya vipaumbele vyake,ambapo amesema anataka kuona katika Mkoa wa Ruvuma,kila mtanzania anakuwa salama na kushiriki ipasavyo bila woga katika uzalishaji mali.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 24,2021   

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.