• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE:Kilimo cha Mkakati kitatatua changamoto ya Mafuta Nchini

Imewekwa kuanzia tarehe: November 19th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia, Jenerali  Wilbert Ibuge amehamasisha kilimo cha Mazao ya Mkakati ili kutatua changamoto ya Uhaba wa Mafuta ya Kula Nchini.

Hayo amesema katika ufunguzi wa mafunzo ya maafisa Ugani  62 katika ngazi ya Mkoa hadi Kata yanayoendelea kwa mda wa siku 3 katika  Ukumbi wa Heltage Msamala Manispaa ya Songea.

Ibuge amesema mafunzo haya ya Maafisa ugani yamelenga kuwajengea uwezo katika kuongeza uzalishaji na tija wa zao la Alizeti   na mazao mengine ya kimkakati na kipaumbele yakiwemo Soya.

“Niwashukuru washiriki wote kwa kuitika wito na kuja kuhudhuria mafunzo rejea ya kanuni za kilimo bora cha zao la Alizeti,Soya na mazao mengine ili kuongeza uzalishaji na tija pamoja na kuongeza upatikanaji wa malighafi kwaajili ya viwanda,Soko la Ndani na nje ya nchi”.

Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo kwa kubadili kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa cha kisasa chenye tija na chakibiashara.

Amesema matumizi ya teknolojia bora,pembejeo bora,mbegu,mbolea na viuatilifu na kuboresha miundo mbinu katika mnyororo wa thamani ili kuzalisha mazao yatakayokidhi  mahitaji ya viwanda vya ndani na ziada kuuzwa nje.

“Wizara imepanga kuboresha huduma za ugani kwa kuwezesha maafisa ugani Kilimo kupata vyombo vya usafiri,mafunzo rejea ya kanuni bora ya kilimo kwa mazao ya Alizeti na Soya pamoja na kuongeza bajeti kutoka milioni 600 2019/2020 hadi kufikia shilingi bilioni 11”.

Mkuu wa Mkoa amesema Serikali imedhamiria katika msimu wa kilimo 2021/2022 kuongeza uzalishaji katika Mikoa yote inayozalisha mazao yenye uhitaji mkubwa katika Soko la ndani na nje ya nchi ili kutekeleza kila afisa ugani kilimo katika ngazi ya Kata na Kijiji awe na Shamba la Mfano shamba darasa ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza kanuni bora za uzalishaji kupitia mashamba.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ugani na Utafiti kutoaka Wizara ya Kilimo Charles Mjema asemea mafunzo haya yametolewa nchi nzima kwa maafisa ugani 1018 wamenufaika katika kanda mbalimbali.

Mjema amesema kwa Mkoa wa Ruvuma maafi ugani 62 wamefanyiwa mafunzo ili kutatua changamoto ya nchi yetu kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi ikiwemo wataalamu wapo,ardhi nzuri ipo pamoja na hali ya hewa na Kanda mbalimbali zinazoweza kuzalisha mazao hayo.

Afisa Ugani Kata ya Ukili  Halmashauri ya Mbinga Mji Hawa Mjiji amesema kupitia mafunzo hayo  wataenda kwa wakulima kuhamasisha na kusimamia katika upandaji wa mazao hayo kitaalamu.

Mjiji ameomba ilikufanya kazi vizuri na kupata matokeo mazuri maafisa ugani wanatakiwa kupatiwa vifaa vya kuandaa mashamba darasa pamoja na shamba la mfano ili wakulima waweze kulima kwa tija na kuvuna kwa wingi.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Novemba 19,2021

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.