• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC MNDEME azindua Kamati ya Maadili ya Mahakimu ngazi ya Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 8th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezindua Kamati ya Maadili ya Mahakimu ngazi ya Mkoa katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mipango wa Mkoa  mjini Songea.

Akizungumza kabla ya kuzindua kamati hiyo,Mndeme amesema mahakimu kama walivyo watumishi wengine wa umma,wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya sheria,kanuni na taratibu za nchi.

“Kwa muda mrefu watumishi wa  kada ya mahakimu wamekuwa wakilalamikiwa kwamba wanakiuka maadili ya kazi yao kwa kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa,matumizi mabaya ya vyeo vyao na kutoa lugha isiyokuwa na staha mbele ya jamii  na kutawaliwa na maslahi binafsi’’,alisisitiza Mndeme.

Hata hivyo Mndeme amesema vitendo  visivyofaa vinavyofanywa na mahakimu wachache wasio waadilifu,vinachafua taswira ya mahakama na kwamba hali hiyo haifai kuacha kuendelea kushamiri.

Amelitaja jukumu kubwa la Kamati  ya Maadili ni kuchunguza malalamiko yanayofikishwa mbele ya kamati na wananchi dhidi ya mahakimu ambapo ametoa rai kwa wajumbe wa kamati hiyo kufanya kazi kwa umoja na mshikamano.

Mndeme amewaomba wananchi kuwasilisha malalamiko yenye ukweli mbele ya kamati ,pia amewaelekeza wakuu wa wilaya zote mkoani Ruvuma,kuunda Kamati za Maadili ya mahakimu ngazi ya wilaya ili kushughulikia malalamiko dhidi ya mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi Kanda ya Songea Jaji Sekela Moshi,akizungumza kwenye uzinduzi huo,amesema mahakimu wana wajibu wa kutoa haki kwa sababu,mahakama imepewa mamlaka ya utoaji haki kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Hata hivyo Jaji Moshi amesema,inapotokea kuna ukosefu wa maadili ikiwemo utovu wa nidhamu,rushwa na mambo mengine,ndipo Kamati ya Maadili ya Mahakimu inachukua nafasi ya kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Amesema kupitia Kamati hiyo,wananchi wataelimishwa utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao ili kupunguza changamoto ya kuwasilisha malalamiko kwenye kamati husika.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki amesema,Kamati ya maadili ni jicho la Tume ya Utumishi wa mahakama katika kusimamia na kuimarisha nidhamu na maadili ya mahakimu.

Kamati ya maadili ya Mahakimu ngazi ya Mkoa inaundwa chini ya kifungu cha 50 cha sheria ya uendeshaji wa mahakama, ikijumuisha Mkuu wa Mkoa,Katibu Tawala wa Mkoa,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa,wakili wa serikali Mfawidhi wa Mkoa na wajumbe wawili walioteuliwa na Jaji.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 8,2020

Songea

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru wamulika maendeleo Nyasa

    May 12, 2025
  • MWENGE wa Uhuru 2025 waikubali miradi yote Mbinga

    May 12, 2025
  • WANANCHI walivyojitokeza kuupokea mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Maguu Mbinga

    May 11, 2025
  • MAHABA ya wananchi wa Mbuji wilayani Mbinga kwa Mwenge wa Uhuru 2025

    May 11, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.