Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi wa shule mpya, ukarabati wa shule kongwe, na upanuzi wa elimu ya juu.
Kanali Abbas amesema hayo wakati anazungumza kwenye kikao cha walimu wakuu wa shule za msingi wapaatao 860 kutoka Halmashauri zote nane kilichofanyika kwenye ukumbi wa Songea Girls
Hata hivyo,Mkuu wa Mkoa amesikitishwa na matokeo mabaya ya kitaifa ya mkoa wa Ruvuma, katika mitihani ya darasa la VII,ambapo Mkoa umefanya vibaya katika masomo ya Hisabati na Sayansi.
Ametoa wito kwa walimu, wakuu wa shule, na mamlaka husika kuboresha hali ya elimu ambapo amesisitiza umuhimu wa walimu kusimamia ufundishaji wa stadi za KKK (Kusoma, Kuandika, Kuhesabu) na kuhakikisha walimu wanatekeleza majukumu yao kwa weledi.
Mkuu wa Mkoa amewaagiza walimu na walimu wakuu kutekeleza majukumu yao kwa umakini, kuzingatia usafi wa mazingira, na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwasaidia walimu katika kazi zao, na aliwataka kuchukua hatua dhidi ya wakuu wa shule wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.
Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mwl.Edith Mpinzile alisema kuwa Mkoa umefaulisha kwa asilimia 69.34 katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2024, ingawa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.28 kutoka mwaka 2023.
Ameitaja sababu kuu inayosababisha Mkoa kufanya vibaya katika matokeo ya kitaifa ya darasa la saba ni kukosa usimamizi katika ufundishaji,alisisitiza kuwa ni muhimu kwa wakuu wa shule kuchukua hatua za kuboresha matokeo ya kitaaluma kwa kuwasimamia walimu.
Hata hivyo alisema Mkoa wa Ruvuma unakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu katika shule za msingi ambapo mahitaji ya Mkoa ni walimu Zaidi ya 10,000,walimu waliopo ni 6,214 na upungufu wa walimu ni 3,815.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.