• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA aagiza milango yote isiyo na viwango iondolewe Kingeritiki na Mbambabay

Imewekwa kuanzia tarehe: February 17th, 2023

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas,ameagiza kuondolewa milango yote iliyofungwa katika Hospitali ya wilaya Nyasa na kituo cha Afya Kingerikiti wilayani humo,baada ya kubaini mbao zilizotumika kutengenezea kutokuwa na ubora unaotakiwa.

Kanal Laban ametoa agizo hilo kwa nyakati tofauti,baada ya kukagua  ujenzi wa kituo cha Afya Kingerikiti ambacho serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 390 kutekeleza mradi huo ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 95 na  ujenzi wa  wodi tatu  katika Hospitali ya wilaya ya Nyasa ambapo serikali imetoa shilingi milioni 800 kutekeleza mradi huo.

Laban,ametoa onyo kali kwa mafundi wanaojenga miradi mbalimbali ya maendeleo na kusisitiza kuwa,mkoa huo sio wa kujifunzia bali ni mkoa unaohitaji mafundi  wenye uwezo na wanaofanya kazi kwa weledi ili miradi inayotekelezwa ilingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

“haiwezekani hata kidogo fundi amekwenda kuokota mabanzi na kuja kutufungia kwenye jengo letu,jambo hili sikubaliani nalo hata kidogo,nakuagiza hakikisha unafanya marekebisho ya milango yote haraka tena kwa gharama zako”alisema.

Alisema,kamwe hawezi kukubaliana na mambo ya ovyo yanayofanywa na  baadhi  ya watendaji wa umma wanaoshindwa kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo yenye lengo la kusukuma kasi ya kukua kwa uchumi wa mkoa huo na kuwataka watumishi wa Halmashauri ya Nya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan,imepeleka zaidi ya Sh.bilioni 1 katika wilaya hiyo kwa ajili ya kujenga vituo viwili vya afya vya Lipalamba na Kingerikiti ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi,hivyo hakuna sababu ya wananchi wa maeneo hayo kuendelea kukosa  huduma.

Aidha Laban, ametoa wiki mbili kwa viongozi wa wilaya ya Nyasa, kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa  kituo cha Afya Kingerikiti ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu.

“hiki kituo kilipaswa kukamilika tangu mwaka jana,lakini naona hadi leo hii ujenzi wake bado haujakamilika,sasa natoa wiki mbili mfanye marekebisho na kianze kutoa huduma”alisema Kanal Laban.

Akiwa katika Hospitali ya wilaya,Kanal Laban amesikitishwa kukuta milango yote inayoendelea kufungwa katika majengo ya kutolea huduma ikiwa imepishana na baadhi mbao zake zikiwa mbichi.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,ameagiza fundi aliyetengeneza milango hiyo kutolipwa fedha hadi atakapofanya marekebisho kwa kuwa amekwenda kinyume na mkataba.

Majengo yanayojengwa ni mochwari,jengo la upasuaji kwa wanawake na wanaume na njia za watembea kwa miguu mradi unaotekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 800 ikiwa ni uendelezaji wa awamu ya tatu ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Filbetho Sanga,amehaidi kufanyia kazi maagizo ya  Mkuu wa mkoa na mapungufu yote yaliyobainika katika ujenzi wa miradi hiyo hasa milango.

Dc Sanga,amewataka wakandarasi wanaofanya  kazi katika wilaya hiyo kuhakikisha kazi wanazofanya zinakuwa bora na hatopokea mradi wowote uliojengwa chini ya kiwango.

Mkazi wa kijiji cha Kingerikiti Zakari Mbele,ameiomba serikali kukamilisha haraka ujenzi wa kituo cha afya Kingerikiti ili waanze kupata huduma za matibabu karibu na makazi yao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.