Pichani Mwenye suti ya kijivu ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas akitoa maekelezo kwa Mkandarasi na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Namabengo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, kuongeza kasi ya ujenzi ambapo kiasi cha shilingi milioni 441 zimetengwa kujenga mabweni mawili, madarasa saba na matundu ya vyoo kumi.
Kanali Thomas amesema Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt, Samia ina lengo la kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu pamoja na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani hivyo ameutaka uongozi wa shule kusimamia ujenzi mchana na usiku ili ifikapo januari ,2024 wanafunzi waweze kutumia majengo hayo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.