MKuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wananchi kuthamini , kuenzi na kuendeleza ngoma asili Mila na Desturi.
Ameyasema hayo Tarehe 16/09/2023 wakati akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa Tamasha la vikundi vya ngoma ya asili ya mganda Kijiji Cha Tumbi Kata ya Kihagara Wilayani Nyasa.
Kanali Thomas ameipongeza Wilaya ya Nyasa Kwa kuendeleleza ngoma za asili za Mganda , kioda na ngoma zingine.
Amefafanua kuwa wananchi tunatakiwa kutunza na kuendeleza utamaduni wa asili Kwa kuwa hakuna nchi ambayo Haina utamaduni.
Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuendeleza utamaduni na kurithisha vizazi vijavyo.
Aidha amewaagiza maafisa utamaduni wa Wilaya ya Nyasa na Mkoa wa Ruvuma kusajili kikundi Cha mganda Cha mwenge ili kiweze kutambulika kisheria na kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.