• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA afungua masoko ya ufuta,soya na mbaazi kupitia mfumo

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed  amefungua masoko ya ufuta,soya na mbaazi kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na TMX wilayani Namtumbo.

Katika uzinduzi wa mnada wa kwanza mkoani Ruvuma katika zao la ufuta jumla ya kilo milioni 1,293,000 zimeuzwa  kwa bei ya wastani wa shilingi  3,903 kwa kilo.

Akizungumza kwenye ufunguzi huo,Kanali Abbas  amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mfumo mzuri wa masoko ya mazao ya wakulima ambapo amesema mfumo huo unaleta manufaa makubwa kwa wakulima.

Amebainisha kuwa ,uendeshaji wa masoko ya zao la ufuta,mbaazi na soya hufanyika kupitia wakulima kununua,kusafirisha na kukusanya mazao kwenye vyama vya msingi 101  vilivyopo katika wilaya za Namtumbo,Songea,Mbinga,Nyasa na Tunduru na vyama vikuu vya ushirika viwili ambavyo ni TAMCU na SONAMCU.

“Mfumo wa stakabadhi ghalani umedhibiti vipimo visivyo halali ambavyo vinamuibia mkulima kwa kuwa mfumo unatumia mizani ya kidijitali ambapo taarifa zote zinakuwa zimehifadhiwa’’,alisema.

Hata hivyo amekemea suala la utoroshaji wa mazao ambapo ameagiza serikali za mitaa kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa mazao na kuziagiza Halmashauri zihakikishe minada inaanza mapema kwa kuzingatia ratiba na kuweka usimamizi Madhubuti wa vyama vya ushirika  katika shughuli zote zinazohusu mifumo ya masoko.

Mkuu wa  Mkoa ameziagiza Halmashauri kuhakikisha zinatoa elimu ya mifumo ya masoko kwa wakulima na wadau wengine ambapo pia amewataka wanunuzi wa mazao na vyama vikuu vya ushirika kuhakikisha wanafanya malipo ya wakulima kwa wakati.

Naye Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Songea na Namtumbo (SONAMCU) Juma Mwanga ametaja hali ya masoko kwa mazao ya ufuta,soya na mbaazi  kuwa inaridhisha ambapo katika kipindi cha miaka minne katika zao la ufuta jumla ya kilo 22,974,950 ziliuzwa na kuingiza Zaidi ya shilingi bilioni 59.

Amesema zao la soya katika kipindi cha miaka minne zimeuzwa kilo 12,915,722  na kuingiza Zaidi ya shilingi bilioni 13 na zao la mbaazi katika kipindi hicho zimeuzwa kilo 13,415,316 ambazo zimeingiza Zaidi ya shilingi bilioni 16.

Ameyataja baadhi ya  mafanikio ya mazao mchanganyiko yaliyouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni wakulima kupata bei nzuri ya mazao,kupungua kwa kiwango cha utoroshaji wa mazao,kuongezeka kwa wanunuzi na kuwepo ushirikiano baina ya wadau wa stakabadhi ghalani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.