MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua tamasha la msimu wa nane la Majimaji selebuka katika viunga vya makumbusho ya majimaji mjini Songea
Akizungumza katika uzinduzi huo amesema tamasha litahusisha mambo mbalimbali ikiwemo kuchochea utalii pia ni fursa muhimu kwa vijana kuibua vipaji.
“Jitihada zinazoongeza thamani ya kuleta tija kama Mkoa ili tuongezeke kimaendeleo zote tutaziunga mkono tangu tulipoanzisha tamasha hili 2014 malengo yake hayajawai kubadilika kila msimu majimaji Selebuka limekua jukwaa la kibiashara la kuwawezesha wajasiliamali kutambulika kwa bidhaa wanazozizalisha”, amesema RC Ibuge.
RC Ibuge amesisitiza wafanyabiashara na wajasiliamali katika tamasha hili muhimu litumike kama kipindi chema cha mavuno na ni fursa ya kuboresha kipato.
Hata hivyo RC Ibuge ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kushiriki Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 2022.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Odo Mwisho amesema mkoa umekuwa mashahidi jinsi unavyo faidika na tamasha hili pia amewapongeza watendaji kwa kutoa matangazo na kuhamasisha
Tamasha la majimaji selebuka linatalajiwa kufanyika tarehe 23 hadi 30 Julai 2022 lengo kuu likiwa kuinua uchumi na kuutangaza utalii wa mkoa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni na Jackson Mbano
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mei 31 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.