MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kupata hati safi miaka minne mfululizo.
Hayo amesema katika kikao maalumu cha Balaza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
“Baada ya pongezi nilizozitoa niseme tena ukweli kuwa matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 Halmashauri ya Madaba mmefanya vizuri sana na mmepata hati safi”.
Hata hivyo ibuge amesema hayo nimatokeo ya utendaji wa kazi nzuri yenye mshikamano na ushirikiano kati ya wataalamu wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na waheshimiwa Madiwani.
“Napenda niwakumbushe kuwa kupata Hati safi miaka mine mfululizo siyo jambo dogo ni jambo kubwa sana tena la mfano Hongereni sana! hivyo naomba niwape shime kwa kupata hati hizo kuwafanye muongeze bidii katika utendaji wa kila siku kwa lengo la kuhakikisha Hati safi zinaendelea kupatikana Madaba”.
Ibuge ametoa maagizo kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha kufunga hoja zote ambazo hazijafungwa kabla ya tarehe 20 septemba 2021 na kupatiwa taarifa kamili ya hoja hizo zilizo jitokeza pamoja na kuzuia hoja zinazojirudia.
Pia wakuu wa Idara washiriki ipasavyo kuandaa majibu ya hoja na utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali,na Halmashauri ichukue hatua ya kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja pamoja na kusimamia mfuko wa Bima ya afya iCHF iliyoboreshwa na kuhakikisha kila mwananchi anajiunga.
Amesema ripoti ya Mkaguzi (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 tunaelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambao unaishia tarehe 30 Juni mwisho wa ukaguzi ni mwanzo wa ukaguzi unaokuja amewasihi kujipanga kwa maandalizi ya ukaguzi bila kupoteza sifa ya kuwa na Hati safi.
Mkuu wa Mkoa ameishukuru ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hususani Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na timu yake kwa ushirikiano wanaotoa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Olaph Pilli akitoa neon la shukrani kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani ameahidi kuendelea kufanya vizuri pamoja na kusimamia miradi ya Halmashauri hiyo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Juni 18,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.