MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametoa Tuzo kwa Halmashauri tatu kati ya nane za Mkoa wa Ruvuma zilizoongoza kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa hoja za CAG .
Halmashauri zilizopewa Tuzo hizo ni za Wilaya ya Mbinga iliyoongoza kwa kuwa na hoja chache kwenye ripoti ya CAG,Halmashauri ya Songea ilioongoza kwa kufunga hoja za CAG na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru iliyokuwa na hoja chache zaidi baada ya zoezi la uhakiki.
Mkuu wa Mkoa amekabidhi Tuzo hizo kwenye kikao cha majumuisho kilichoshirikisha viongozi na watendaji kutoka Halmashauri zote na kufanyika kwenye ukumbi wa Skyway mjini Tunduru
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.