MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed,amefunga Bonanza la Eid lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea ambalo wanamichezo wa mkoa huo walitumia bonanza hilo kumkaribisha rasmi mkoani Ruvuma.
Bonanza hilo lilishirikisha timu tano za mpira wa miguu ambapo Timu ya Kazaroho Veterani iliibuka mabingwa baada ya kuwafunga wapinzani wao wakubwa Timu ya Songea Pamoja Goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali na kujinyakulia kombe na fedha taslimu Sh.laki tano huku Timu ya Songea Pamoja iliyoshika nafasi ya pili ikipata zawadi ya jezi.
Timu za mpira wa miguu zilizoshiriki bonanza hilo ni Kazaroho,Songea Pamoja,Peramiho Veterani, Songea Veterani na Uvccm Ruvuma,ambapo wana muziki wa kizazi kipya na wasanii wa ngoma za asili wa mkoa wa Ruvuma walitoa burudani kwa wananchi waliofika katika uwanja wa Majimaji.
Kwa upande wa Netiball, timu ya Uvccm wilaya ya Songea iliibuka mshindi wa jumla baada ya kuzifunga timu nyingine nne zilizoshiriki kwenye Bonanza hilo ikiwemo KazaRoho Queen na kupata Sh.laki moja na timu washiriki wa bonanza hilo zilipata jezi seti moja kila moja.
Akizungumza na wananchi na wana michezo walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu wa mkoa,amewapongeza wana michezo walioshiriki na wadau waliowezesha kufanyika kwa bonanza hilo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani na kusherehekea Sikukuu ya Eid.
Mkuu wa mkoa,amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya michezo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.