Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameongoza kikao cha Baraza la Biashara cha Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao hicho, Kanali Ahmed aliwapongeza wafanyabiashara kwa mchango wao mkubwa katika kukuza pato la Mkoa na Taifa.
Alisisitiza kuwa Baraza hilo ni jukwaa muhimu la majadiliano kati ya sekta binafsi na Serikali, likilenga kutatua changamoto na kuboresha mazingira ya biashara.
Hata hivyo amewaagiza watendaji serikalini katika ngazi zote kuhakikisha Baraza hilo linafanyika kila mwaka kwa mujibu wa mwongozo.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo alibainisha kuwa biashara ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi, akiahidi ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuimarisha uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Kudrack Darajani aliwasilisha maombi ya wafanyabiashara, yakiwemo VAT kutozwa viwandani na mipakani, kufutwa kwa faini za mashine za EFD, na kuwekwa uwazi katika makadirio ya mapato.
Pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.