MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amepiga marufuku ufuvi wa Dagaa wadogo ambao hawaleti tija kibiashara.
Hayo amezungumza alipotembelea Kata ya Mbambabei Wilaya ya Nyasa amesema uvuvi haramu unasababisha kupoteza upatikanaji wa dagaa ambao wanaleta faida kwa wananchi.
“Wale tuliokwenda Nane nane tumeuza Dagaa dumla moja shilingi elfu 25,000/= hiyo ni kwaajili ya faida yenu na nilisema dagaa wasiuzwe shini ya shilingi elfu 15,000/=”.
Amesema atasimamia wote wanao dhurumu maslahi ya watu hivyo ameomba Mazalia ya Dagaa wadogo waashwe wakue ili wauzwe kwa faida ya wananchi.
Thomas amesema ifike wakati Dagaa wa Ziwa Nyasa wauzwe kwa mnada siyo kila mtu ananunua kiholela kwa wale ambao wanataka kudhurumu wananchi wachukuliwe hatua.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Eng.Stella Manyanya amelaani uvuvi amesema kwa masikitiko Makubwa juu ya Uvuvi huo haramu wa kuvua Dagaa wadogo.
Manyanya amesema ni wadau wake katika swala zima la kumpigia Kura kupitia hilo amesema hawezi kunyamaza wala kuunga Mkono.
“Wenzetu Nchi za Jirani zilizopakana na Wilaya ya Nyasa hawavui Samaki na Dagaa wa Dogo inawasaidia kuvua kwa tija na kuongeza mapato.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 19,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.