• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA apongeza ujenzi wa hospitali ya Manispaa ya Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: October 24th, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewapongeza wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya Manispaa ya Songea iliyopo eneo la Sanangula, Kata ya Shule ya Tanga.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua maendeleo ya Hospitali hiyo ambapo amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya ujenzi na kuhakikisha kazi  zinamalizika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika eneo la karibu.

"Nimekuja kuona utekelezaji wa miradi ndani ya Mkoa wetu wa Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kwamba ikifika Disemba miradi mingi iliyopatiwa fedha iwe imekamilika," alisema Kanali Ahmed.

Amewataka watumishi wa hospitali hiyo kutoa huduma zinazolingana na taaluma yao kama wahudumu wa afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesisitiza kuwa mtaalam wa afya anatakiwa kuwa na huruma, kutoa huduma bora kwa wagonjwa na mwenye kujali, hivyo amewataka kuyazingatia hayo ili wananchi wanapoenda kupata huduma waone wapo kwenye eneo salama na sio eneo la manyanyaso.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dkt. Amos Mwenda amesema mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe 9  Disemba 2021 na hadi kufikia Septemba 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea Shiningi Bilioni 1.1 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Ameongeza kuwa mradi huo uliibuliwa na wananchi wa kata ya Shule ya Tanga kupitia mpango wa fursa na vikwazo ili kupunguza kero na umbali wa upatikanaji wa huduma za afya.

Awali wananchi wa kata ya Shule ya Tanga walilazimika kutembea kwa umbali wa takribani kilometa 20 kufuata huduma za afya katika kituo cha afya cha Mjimwema na hospitali ya Rufaa ya Mkoa ,Songea

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.