Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas ametoa wito kwa uongozi wa madereva bodaboda na bajaji wahakikishe wanachama wao wanakuwa na leseni na kufuata sheria za usalama barabarani.
Kanali Thomas ametoa wito huo wakati anazungumza katika kikao cha wajasiriamali wadogo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea kikihusisha makundi ya wamachinga,waendesha bajaji na bodaboda .
Amewashauri madereva bodaboda na bajaji watumie lugha nzuri yenye ushawishi kwa wateja na kuzingatia usafi wa mwili na mavazi na kwamba wasikubali kutumiwa vibaya kwenye vitendo viovu .
“Viongozi ambao tumechaguliwa na kuaminiwa katika ngazi zote tuweke ratiba ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ”,alisisitiza RC Thomas.
Awali Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Ruvuma Salum Masamaki amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo kuwa ni miundombinu mibovu ya barabara katika baadhi ya barabara na miundombinu mibovu kwenye masoko ya songea mjini.
Katika kikao hicho Kanali Thomas ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko kutatua kero na changamoto kwa bajaji na bodaboda zinazotokana na kuombwa rushwa na baadhi ya mgambo wanaopita katika maeneo yao na kukarabati miundombinu ya barabara na masoko.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anaendelea na ziara ya kukutana na makundi mbalimbali ili kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.