Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas amewahimiza wananchi mkoani umo kuwekeza kwenye kilimo cha miti kwani kinatija na uhakika wa kukopesheka na taasisi za fedha
Kanali Thomas ameyasema hayo hivi karibuni alipo shiriki hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi na nyumba tatu za watumishi katika shamba la miti Mpepo linalohudumiwa na wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
Amesema kilimo ambacho kinaondoa umasikini kwa haraka lakini kinahitaji subira ni kilimo cha upandaji wa miti ambacho uvunaji wake uchukua miaka kumi hadi kumi na tano pia baada vunaji hapo ndipo watakapoona faida kubwa ambayo imelala kwenye miti
“Niwaombe tusiwe watazamaji wakati (TFS) wanapanda miti na sisi tuwe sehemeu ya wanufaika kwa kupanda miti kwani kufanya hivyo ndipo tutakapoona uchungu wa kuchoma miti kila wakati” amesema Kanali Thomas.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.