• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA atahadharisha kuhusu ushoga,ataka wanawake wasiwe chanzo cha udhalilishaji

Imewekwa kuanzia tarehe: March 9th, 2023

MKUU  wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas,amekemea tabia ya baadhi ya wanawake hapa nchini, kuwa chanzo cha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo ushoga tabia inayozidi kuongezeka katika jamii.

Kanal Laban ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza na wananchi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa imefanyika katika viwanja vya Bandari katika mji mdogo wa Mbambabay wilayani Nyasa.

Amewataka wanawake katika mkoa huo kushirikiana na kusaidia  katika shughuli mbalimbali ili kujiletea maendeleo yao.

Kanal Laban, amewaonya  kuacha  tabia ya kuchukiana miongoni mwao kwa kuwa inawarudisha nyuma na kuwapunguzia nguvu pale wanapodai haki zao za msingi katika vyombo vya maamuzi,sehemu za kazi na  katika jamii inayowazunguka.

Aidha Mkuu wa mkoa alisema,serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imesimama kidete kwa kutetea na kutoa haki kwa wanawake hapa nchini na kuwapa fursa na nafasi mbalimbali za uongozi na kwenye vyombo vya maamuzi.

Amewaomba wananchi hususani wanawake katika mkoa huo kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinavyotokea katika jamii zao ili serikali iweze kuchukua hatua sitahiki.

Mkuu wa mkoa aliongeza kuwa,jumla ya shilingi milioni 588,252.2 zimetolewa kwa vikundi 93 kutoka mapatao ya ndani ya Halmashauri za mkoa wa Ruvuma ambazo zimewezesha wananchi  waliomo kwenye makundi maalum ya vijana,wanawake na wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi.

Awali katika risala yao iliyosomwa na Mariam Juma,wanawake  wa mkoa huo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutambua mchango wa wanawake na kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zimewezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuondokana  katika umaskini.

Wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuwawezesha wanawake kuonekana kwenye maeneo mbalimbali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii kwa ujumla.Hata hivyo alisema,bado kuna kundi kubwa la wanawake limeachwa nyuma kutokana na rasilimali chache zinazopatikana ikilinganishwa na idadi ya wanawake waliopo.

Ameiomba serikali  kulitupia macho kundi hilo na kushauri wanawake washirikishwe katika nafasi za maamuzi na kutatua changamoto zao kwenye maeneo na kutolea mfano utambuzi wa haki zao za msingi katika maeneo wanayoishi.

Juma ametolea mfano wanawake wa mkoa wa Ruvuma kuwa ndiyo wazalishaji wakuu wa mazao ya chakula na biashara,lakini mara nyingi hawashirikishwi katika kupanga matumizi ya kile kinachozalishwa.

Alisema,jambo hilo limepunguza ari ya kufanya kazi kwa bidii hasa ya uzalishaji mali na hatimaye kusababisha uchumi wa kaya husika kudorora, tofauti na kaya ambazo wanashirikiana katika kupanga mipango bora ya maendeleo.

Ameishauri serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,kutilia mkazo  mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani inayotolewa na Halmashauri za wilaya kwa makundi maalum ya wanawake,vijana na walemavu itolewe kwa wakati ili iweze kusaidia katika kukuza mitaji na kuongeza kipato cha familia.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo alisema,baadhi ya wanawake wanakosa huduma muhimu kutoka kwa waume zao kwa sababu ya wanaume kutumia muda wao mwingi wakiwa katika starehe.

Alisema,tabia hiyo imeleta maumivu makubwa kwa wanawake wengi  na wengine wamekata tamaa na hata kujilaumu kwa kukubali kuingia kwenye ndoa ambazo zimepelekea kupata maumivu makubwa na kukosa furaha ,amani na utulivu katika maisha yao.

Mangosongo,amewataka wanaume kubadili  na kusaidiana na wanawake kulea familia zao ili kujenga familia bora na kuwa na kizazi chenye furaha na utulivu wakati wote.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.