MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka viongozi wa Kata pamoja na Halmashauri kuwashirikisha wananchi kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo kwani itasahidia wananchi kuacha kuhujum miradi hiyo
Hayo ameyasema wakati akizungumza katika mjumuisho wa ziara yake aliyoifanya kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Songea kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Lizaboni, Chandarua na Matogoro
Amesema Serikali imetoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 75 kwa lengo la kuondoa upungufu wa madarasa hivyo miradi kama hiyo ni vyema wananchi washirikishwe moja kwa moja maana itasahidia na wao kulinda mradi hiyo
Lakini sehemu nyingi tunazopita tunakuta kamati nyingi hazihusishi wananchi kwahiyo inapelekea wananchi kutokujua taarifa za fedha kuhusu miradi badala yake wanaitwa kubeba tofali asa ili wananchi wasiwe sehemu ya kuhujum mradi lazima washirikishwe kwani itamkumbusha Zaidi kuukinda mradi
Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa viongozi wa Halmashauri wasipende kutelekeza miradi kwa wakandarasi bila kutembelea kwani inaleta shida kwenye usimamiz wa matumizi wa fedha na vifaa pia kusababisha miradi kutokamilika kwa wakati na kufanya jitihada za serikali kukwama
Mara chache sana kiongozi kutembelea miradi bila kuulizwa na mkubwa wake ni wasisitize fedha zote zilizopo kwenye miradi tusiache kuja na kuitembelea na lakini kuitolea taarifa ili inapojitokeza changamoto tuifahamu mapema
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe, Pololet Mgema amemshukuru Rais Samia kwa kuwaleta fedha hizo za ujenzi wa madarasa 75 pia ameahidi kusimamia utekelezaji kwa kushirikiana na wananchi ili kutimiza lengo la Serikali
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.