MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameongea na wazee wa Wilaya ya Nyasa kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kutatua.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Veta amesema Mkoa umeunda balaza la wazee litakalosaidia kufikisha changamoto za wazee kwa kuraisi.
“Kuishi ni haki yenu,kupata matibabu ni haki yenu na nyie mmekuwa wazalishaji wa kubwa katika kilimo mlikuwa mkiniletea chakula nawashukuru sana”.
Thomas ametoa rai kwa Kiongozi wa Balaza la wazee kwa kuwatumia wazee wa Wilaya ya Nyasa waunde balaza litakalo toa haki kwa wazee hao na kutatua migogoro itakayojitokeza.
Hata hivyo amaewaomba wazee hao kuhakikisha wanalea vijana katika maadaili na mienendo bora itakayosaidia kuwa na Taifa lenye vijana wazalendo na wachapakazi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga akikaimu Wilaya ya Nyasa Aziza Mangosongo amesema Wilaya ya Nyasa inawazee 1, 820 ikiwa wazee 4020 wanakadi za matibabu bure na wazee 3,508 bado hawana kadi za matibabu.
Amesema Wilaya ya Nyasa ina kaya 8218 na katika idadi hiyo kuna Wazee wanaonufaika na mpango wa TASAF.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 21,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.