• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA awachangia wamachinga mifuko 50 ya saruji

Imewekwa kuanzia tarehe: January 31st, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewahaidi wamachinga wa Manispaa ya Songea kuchangia mifuko 50 ya saruji na kugharamia uchimbaji shimo la choo chao.

Kanali Thomas ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza baada ya kusikiliza kero mbalimbali za  wamachinga katika viunga vya Soko la Majengo Mjini Songea.

Amesema hapendi kuwaona wamachinga wanafanya biashara kwenye mazingira magumu ambapo amewataka wamachinga wote kufanya biashara kwenye maeneo waliyotengewa na serikali.

 Kanali Thomas amewaomba wafanya biashara kuwa wazalendo katika kutoa pesa  za kuchangia gharama za kuzolea taka Kwa mzabuni wao ili kuweka mazingira safi na salama ya Soko na mji wa Songea kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Kanali Thomas amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko kuwakamata watoto wa shule wanafanya biashara sokoni na Kwenda kuwaonesha wafanyabiashara wanaowatumikisha kufanya biashara  badala ya Kwenda shule.

Katika kikao hicho  Mkuu wa Mkoa amemuuagiza Mwakilishi wa Meneja wa NMB Noela Minja kuendelea kutoa mikopo na elimu ya biashara  kwa wamachinga ili wakuze biashara zao.

Minja amesema Benki ya NMB hadi sasa   imetoa mikopo  kwa wamachinga 35 ambao wamekidhi vigezo vya kupata mikopo,Meneja huyo pia  ameahidi  kutoa shilingi  100,000 kuchangia ujenzi wa choo cha wamachinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko amehaidi katika ujenzi wa choo hicho kutoa bati na malipo ya fundi ili kukamilisha ujenzi kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa TANESCO Mashauri Adamu ameahidi kuchangia shilingi 300,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wamachinga.

Awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wadogo Mkoa wa Ruvuma Salum Masamaki amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufika kusikiliza kero za wamachinga na kuzitafutia ufumbuzi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.