MKUU wa Mkoa wa Ruvuma ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kuzungumza na watumishi kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akisoma taarifa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo amesema kuna changamoto ya watumishi katika idaraya Elimu Msingi na Sekondari uhitaji ni watumishi 2,248 waliopo ni 978,upungufu 1,270 kwa Shule za Msingi na Sekondari uhitaji ni 881 waliopo ni 504 upungufu 377.
Amesema katika idara ya Afya kuna uhitaji wa watumishi 777 waliopo ni 241 upungufu ni 536 kilimo na Uvuvi uhitaji 158 waliopo 456 ikiwemo idara zingine kuwa na upungu.
“Jumla ya watumishi 166 walipandishwa vyeo kwa Mwaka 2021 -2022 watumishi 68 zoezi la kupandisha vyeo linaendelea”.
Mangosongo amesema katika ajira mpya Halmashauri imepokea watumishi 256 katika kada ya Elimu ya msingi walimu 40 Sekondari 48 Afya 22 na wote wameripoti .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza na watumishi hao amesema katika utumishi kila mtu anawajibu wake katika utendaji wa kazi ya Serikali bila kujali upungu wa watumishi uliopo.
Thomas amesisitiza mahusiano mazuri kazini bila kutoa siri za ofisi pamoja na kuheshimiana maeneo ya kazi yanasababisha kuto kuwa na majungu ambayo hayana tija katika utendaji.
“Mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na nisingekuwa na mahusiano mazuri na wenzangu leo nisingepewa ushirikiano mzuri katika utendaji kazi”.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa watumishi hao katika ukusanyaji wa mapato kuwa waaminifu kwa mfumo wa POS na kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa sehemu husika kwa wakati bila kuhujumu Serikali.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza kilimo cha pamoja ikifuatia kwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kutoa Mbolea ya Ruzuku amabyo itasaidia wakulima unafuu wa pembejeo.
“Rais Samia ametoa Mbolea za Ruzuku twende tukasimamie watu wengi wasajiliwe zoezi lisimamiwe liwe endelevu bila upendeleo ”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 20,202
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.