Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewakabidhi wakuu wa Wilaya watatu magari mapya ya kisasa yaliyonunuliwa na serikali.
Hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea ambapo wakuu wa Wilaya za Tunduru,Mbinga na Namtumbo wamekabidhiwa magari hayo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa wa fedha uliosababisha kupatikana kwa vifaa vya usafiri ambavyo vinakwenda kutumika na wakuu wa Wilaya.
Amesema kwa kuanzia serikali ilitenga bajeti ya kununua magari mapya kwa wakuu wa wilaya watatu ambao walikuwa na changamoto kubwa ya magari ambapo amewatia moyo wakuu wa wilaya ambao hawajapata magari mapya kuwataka wawe na Subira kwa kuwa serikali itaendelea kutenga bajeti ya ,kununua magari.
“Magari haya yamenunuliwa kwa fedha nyingi,hivyo thamani ya fedha inatakiwa kuakisi thamani ya fedha iliyotumika kwa kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao,wananchi wanatamani kuona changamoto zinazowakabili zinatatuliwa’’,alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya akizungumza kwenye hafla hiyo,amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kununulia magari kwa wakuu wa wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
Amesema ukosefu wa magari kilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wakuu wa wilaya ambapo iliwalazimu wakati mwingine kuazima magari kwa wakuu wa Idara ili Kwenda kutatu changamoto kwa wananchi.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge aliyataja magari mapya yaliyonunuliwa na serikali kuwa ni gari lenye namba STN 2928 ambalo limenunuliwa kwa ajili ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,gari STN 2929 kwa ajili ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga na STN 2927 kwa ajili ya Wilaya ya Namtumbo.
Madenge amesema magari hayo yatawasaidia wakuu wa Wilaya hizo kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya ufuatiliaji na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi
vijijini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.