• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC Ruvuma awaongoza wananchi kuaga waliopoteza maisha kwa ajali Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: January 3rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewaongoza wananchi  kuaga miili ya watu sita waliopoteza maisha kwenye ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Chunya Wilayani Mbinga.

Tukio hilo limefanyika katika uwanja wa michezo wa CCM uliopo Halmashauri ya Mji wa Mbinga na kukabidhi miili hiyo kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya kufanya maziko.

Akitoa salamu za pole wakati wa kuaga miili hiyo, Kanali Ahmed, amesema hiki ni kipindi kigumu na kinachoumiza hasa unapoangalia aina ya kifo kilichotokea, amewapa pole waliowapoteza wapendwa wao na kuwasihi watu wote kutumia msiba huo kutafakari maneno ya viongozi wa dini, kujiandaa kwa kusali, kufanya toba, na kushiriki kwenye matukio kama hayo kwa kuwa hakuna ajuaye siku wala saa.

"Kuagana kwa aina hii hakuleti faraja hata siku moja,  unaagana na mtu ambaye huwezi tena kukutana naye, ni kipindi kigumu, ni kipindi kinaumiza, kinaumiza zaidi unapoangalia aina ya kifo kilivyotokea, ndugu zetu hawa hawakuwa hata na dakika moja ya kujitetea, baadhi yao ni vijana wadogo walikuwa wana ndoto zao binafsi lakini Taifa lilikuwa lina ndoto kubwa dhidi yao, nimeyapokea haya kwa maumivu makubwa sana, na kwa idadi hii Mkoa na Taifa limepoteza nguvu kazi,"  alisema Kanali Ahmed.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema kutokana na ajali hiyo Shule ya Msingi Lumalu iliyokuwa na walimu watano imepoteza walimu wanne, hivyo watalifanyia kazi swala hilo ili wapate walimu wengine kwaajili ya kuendelea kutoa huduma shuleni hapo.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komred Oddo Mwisho, amesema wananchi sita kuondoka kwa wakati mmoja ni idadi kubwa sana wakati bado walikuwa wanahitajika kulitumikia Taifa, hivyo Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa kwa kuondokewa na nguvu kazi kubwa na aina ya kifo kilichowapata.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori amesema anaweza kuhisi maumivu wanayopata wafiwa Kwa kuwa wapo waliopoteza wazazi, watoto na wengine wake, amesema neno la Mungu likawape faraja wafiwa hao katika kipindi kigumu wanachopitia.

Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu sita ilitokea Disemba 28, 2024 katika kijiji cha Chunya wilayani Mbinga ilihusisha gari ndogo aina ya Prado ( T 647 CVR ) baada ya kupinduka na kuwaka moto, waliopoteza maisha ni walimu wanne wa shule ya msingi Lumalu ambao ni Damas Damasi Nambombe, Dominika Abehart Ndau, Judith Joseph Nyoni na John Silvester Mtuhi, dereva wa gari hiyo Vincent Alex Milinga pamoja na Raia mmoja Bonface Bosco Mapunda.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.