Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Ruvuma wanakuwa sehemu ya kupata huduma ya maji safi na salama
Kanali Thomas ameyasema hayo wakati akitao salam za Mkoa kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika Mji wa songea, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Mtarawe Machi 10, 2023 Manispaa ya Songea
“Mkoa wa Ruvuma umepiga hatua kubwa katika utoaji huduma ya maji safi na salama ambapo hadi sasa utoaji huduma ya maji mijini umefikia asilimia 80.95 ambapo katika Halmashuri ya Manispaa ya Songea umefikia zaidi ya asilimia 90 na utoaji wa maji mjini Songea ni saa 22 kwa siku.”
Hata hivyo amesema upatikanaji wa maji vijijini mkoani Ruvuma,kati ya vijiji 525 vilivyopo mkoani Ruvuma.vijiji 355 vinapata maji safi na salama sawana asilimia 67.
“Pamoja na mradi huu unaoenda kutelezwa pia kwa mwaka huu wa fedha 22/23 Mkoa wa Ruvuma umetengewa kiasi cha bilioni 16.5 kwa ajili ya utelezaji wa miradi mbalimbali ya maji, aidha mkoa unaendelea kutekeleza miradi 33 yenye jumla ya bilioni 51.2”
Mkataba wa ujenzi wa mradi huo ni wa miezi 32 kuanzia Machi 10,2023,kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea kutaleta manufaa makubwa ikiwemo SOUWASA kuongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka lita milioni 11.58 kwa siku hadi kufikia lita milioni 42.581 kwa siku,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.