Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Kampuni ya Gewa General Enterprises ya Morogoro kwa kutumia teknolojia rahisi ya mawe kujenga daraja la mawe katika barabara ya Lipupuma-Mgombezi-Chechengu Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea lililogharimu shilingi milioni 153 badala ya milioni 500.
Kanali Thomas ametoa pongezi hizo baada ya kukagua mradi huo uliotekelezwa na TARURA huku akisisitiza teknolojia hiyo kutumika kutekeleza miradi ya madaraja ili kuokoa fedha za serikali ambazo zinaweza kutumika kwenye miradi mingine.
Daraja hilo linalounganisha vijiji vya Lipupuma,Mgombezi na Chechengu limekuwa ukombozi kwa wananchi wa vijiji hivyo vinavyozalisha kwa wingi zao tangawizi na mbao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.