MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemtaka mkandarasi wa kampuni Associates LTD kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Matomondo-Mlale JKT, ambayo inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Hayo ameyasema wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa barabara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni 4 kipitia fedha za Tozo ya mafuta kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kilomita 3.5 za lami na ujenzi wa barabara ya changarawe kilomita 19.0
Kanali Thomas alisema Mhe, Rais ametoa Zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi kipande cha barabara ya lami nyepesi kwa urefu wa kilomota 3.5 ili kuwaondolea wananchi wake changamoto mbalimabali za kiusafiri asa wakati wa masikia
“Kama tulivyo toka kupata ushuhuda kwa Wananchi ni kweli Mhe, Rais ametoa fedha hizo lakini leo nitazungumzia ujenzi wa kipande cha lami sababu lami itakuwa mkombozi kwa wananchi hawa lakini niwajibu wetu sisi kama wataalamu kuhakikisha tunasimamia miradi kama hii kuisha kwa wakati”,alisema Thomas
Hata hivyo amemsisitiza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo tena kujenga kwa kiwango kinachotakiwa kwani mkataba wa ujenzi huo unatarajia kukamilika tarehe 14 /12/2022 pia amewataka Wananchi kuendeke kusimamia na kulinda ujenzi huo wa Barabara
Naye Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Wahabu Yahaya Nyamzungu akikosoma taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa Ruvuna na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe, Pololet Mgema, alisema mradi huo umefikia asilimia 65 za utekelezaji
“TARURA imeingia mkataba wa ujenzi wa barabara ya Matomondo-Mlale JKT na mkandarasi BR/ ASSOCIATES kwa gramaha ya shilingi Bilioni 4 kwa namba ya mkataba AE/092/2021-2022/HQ/CR/17. Mkataba ulianza tarehe 14/04/2022 na unatarajia kumalizika tarehe 14/12/2022”alisema Nyamzungu
Pia maeleza kuwa TARURA itaendelea kumwelekeza mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi kipindi cha kiangazi vile vile kufanya mapitio ya mkataba yanaendelea ili kuwezesha ujenzi wa kalavati, boksi na tabaka la CRS unafanyika kwa wakati
Naye Agnes Ngonyani ambaye ni katibu wa chama cha mapinduzi kijiji cha Matomondo amemshukuru Mhe, Rais kwa jitihada za kuwaboreshea barabara hiyo amaboyo kukamlika kwake itafungua fursa kama kukuwa kwa mzunguko wa biashara na usafiri wa uhakika
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.