Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametembelea mafunzo Makarani na wasimamizi wa Maudhui ya sensa ya watu na makazi.
Akizungumza katika ukumbi wa mafunzo katika vituo vya Manispaa ya Songea na Songea vijijini Songea ametoa rai kwa Makarani hao kukusanya taarifa sahihi pamoja na kutunza siri.
"Zoezi hili linafanyika mara moja kila baada ya miaka kumi taarifa mtakazozikusanya zitatumika kwa muda wa miaka kumi hivyo hakikisheni mnapata data zote za wananchi ikiwemo za walemavu ".
Thomas amewataka makarani na wasimamizi wa maudhui kuacha kutumia vishikwambi kwa matumizi ambayo siyo sahihi kwenye vishikwambi walivyopewa na serikali kwaajili ya ukusanyaji wa taarifa za Sensa.
"Mmepewa vishikwambi kwaajili ya kazi maalumu ambayo ni kwaajili ya sensa ya watu na makazi,hivyo epukeni matumizi yasiyo sahihi kama kupiga picha kuingia kwenye mitandao ya kijamii”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi itakayo fanyika Agosti 23 2022 ili serikali iweze kuweka mipango bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amewataka makarani na wasimamizi wa maudhui kufanya kazi kwa uzalendo
“akikisheni mnatumia nafasi hii nyeti kabisa kuhakikisha mnatekeleza zoezi hili la kitaifa kwa uaminifu na kwakua wazalendo”
Imeandaliwa na Janeth Ndunguru
Kutoka kitengo cha mawasiliano ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma
Agosti 12 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.