Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametoa rai kwa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium kuhifadhi Mazingira
Rai hiyo ameitoa wakati Akizungumza na Viongozi wa kampuni hiyo alipotembelea katika kambi pamoja na maeneo ya mgodini yaliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma
Amesema uchimbaji wa madini hayo upo tofauti sana na aina nyingine za madini hivyo kama Serikali ya Mkoa haiwezi kiruhusu wachimbaji wadogo wadogo kujihusisha na ujimbaji wa madini hayo kwani Uranium uchimbwa kitaalamu kama ilivyo elezwa na wataalamu
“Lakini rai yangu kwenu tuzingatie sana utunzaji wa mazingira tumeona sehemu kubwa imesafishwa kwa ajili ya uchimbaji niwatake mzingatie shughuli zenu zisije kuaribu mazingira hicho ndio kitu cha muhimu na tuzingatie maana tumelithishwa tuwalithishe”amesema Kanali Thomas
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.