Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka baadhi ya watumishi wa vituo Afya Wilaya ya Mbinga kutumia lugha nzuri kwa wazee
Kanali Thomas ameyasema hayo wakati alipokutana na Wazee wilayani umo akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na kuzungumza Watumishi wa umma katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Aziza Mangasongo, alisema Serikali kila mwaka ya inatenga bajeti ya kununua dawa kwaajili wananchi watibiwe na taarifa ya Wilaya inaonyesha dawa zinapatina Zaidi ya asilimia 90 asa kwanini Wazee wanambiwa wakanunue dawa madukani
“Wakati mwingine kinachotibu sio dawa pekee yake ni kauli tu je Unapokelewaje unamjali vipi mgonjwa muda mwingine kauli nzuri inatibu kabla ya kuanza matibabu, mbele ya Wazee hawa nakutaka katibu wa Afya uwaambie watumishi wako wabadilishe lugha asa kwa wazee watumie lugah nzuri” alisema Kanali Laban.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.