Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiongea na wanafunzi wa darasa la kwanza ambao wameripoti kujiunga na Elimu ya msingi katika shule mpya ya msingi Lipupuma iliyopo Halmashauri ya Madaba
Kanali Thomas amewataka wazazi na walezi ambao hadi sasa bado awajawapeleka watoto wao kuwaandikishwa kujiunga na elimu ya Awali, Msingi na waliofaulu kujiunga na Sekondari kuwaandikisha mara moja kwani serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imewezesha mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia.
Amesema Serikali imetimiza wajibu wake kwa kutoa elimu bila malipo hiyo wazazi na walezi nao wanatakiwa wawajibike kwenye nafasi zao kwa kununua sare na mahitaji ya shule yanayohitajika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.