MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezungumza na watumishi wa Ofisi yake.
Akizungumza na watumishi hao katika ukumbi wa Songea Clab Manispaa ya Songea ametoa rai kwa watumishi kuwa na ushirikiano katika utendaji kazi ili kuhakikisha Ruvuma inaendelea kushika nafasi ya utendaji bora.
“Ninaomba tuzidishe mahusiano mazuri katika utendaji kazi mimi siyo muumini wa majungu na makundi tufanye kazi”.
Thomas amesema kwa dhamana ya utumishi waliyopewa ya utumishi Serikalini muitendee haki katika kuwatumikia wananchi na kushirikiana katika kazi bila kuangalia nani unamdumia.
Hata hivyo amesema wakuu wa Idara na Vitengo watoe ushirikiano bila kuonekana miiungu watu usawa na uzalendo uonekane ili kuhakikisha tunakuwa na timu bora.
“Kwenye idara na vitengo kuna watu wapo peponi wengine motoni wanasafiri wao tu wote tumekuja kutafuta pesa “.
Amesema kwa mtumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa atambue kuwa ni msimamizi wa Mkoa mzima hivyo waache kufanya kazi kwa kuwaogopa viongozi wakiwepo ofisini kazi zinafanyika wasipokuwepo watu wanatoroka kwenda kufanya shughuli zao.
“Kila mtu atambue amekuja hapa kufanya kazi kwa dhamana aliyopewa na tambueni mtaani kuna watu wengi wanaelimu kubwa kushindwa sisi wanazitamani hizi nafasi”.
Mkuu wa Mkoa amesisi tiza katika swala zima la kuhakikisha watumishi wanatunza wazazi wao kuacha kufanya mambo ya hovyo ambayo yasababisha kutopata Baraka.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 10,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.